Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, ndege iliyokuwa imebeba mwili wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Shahidi Sayyid Ali Khamenei, iliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Najaf Ashraf huku ikipokelewa kwa uwepo rasmi na mpana wa viongozi, maafisa na watu mbalimbali wa nchi mbili za Iraq na Iran, akiwemo Waziri Mkuu wa Iraq.
Mwili wa Shahidi ulihamishwa kutoka ndani ya ndege hadi katika eneo la uwanja wa ndege, ambapo umati mkubwa wa watu ulianza kuusindikiza mwili huo mtukufu. Baada ya hapo, hafla ya mazishi ya wananchi ilitarajiwa kuanza saa kumi na mbili asubuhi (06:00) siku ya Jumatano kuelekea kwenye Haram Tukufu ya Amirul-Muuminina, Imam Ali (as). Kisha, mazishi hayo yaliendelea kuelekea Karbala Tukufu, yakihudhuriwa na mamilioni ya wananchi kutoka mikoa mbalimbali ya Iraq na kutoka nchi tofauti.

Maoni yako